Taarifa kwa Umma

Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, yaani MUHAS Academic Medical Centre (MAMC) iliyopo katika Kampasi ya Mloganzila ni hospitali ya kisasa na yenye vifaa tiba vya kisasa. MAMC ilianza kutoa huduma kwa wagonjwa tarehe 18 Septemba 2017 kwa kutoa huduma za kliniki za madaktari bingwa kwa wagonjwa wa nje (Outpatient Department Clinics) pamoja na huduma katika kitengo cha magonjwa ya dharura (Emergency Medicine Department). Huduma za kulaza wagonjwa zilianza tarehe 20 Novemba 2017 kwa kuanza kutoa huduma kwa wagonjwa wa kulazwa katika vitengo vya magonjwa ya ndani (Internal Medicine) na watoto. Hospitali hii ilifunguliwa rasmi na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli tarehe 25 Novemba 2017.
Baada ya kufunguliwa, MAMC pia imeendelea kupokea wagonjwa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili hususani kutoka katika kitengo cha magonjwa ya ndani, pamoja na hospitali za Rufaa za Mkoa wa Dar es Salaam, Tumbi na nyinginezo hapa nchini. Soma zaidi..

Application for Postgraduate Degree Programmes for Academic Year 2018/2019

Applications are invited from the public for postgraduate degree studies at the Muhimbili University of Health and Allied Sciences. For more information and application procedures, Please Click Here. Applicants for Postgraduate Programs are required to apply online. Click here to apply
Deadline for submitting applications is Saturday 31st March, 2018    

Loading ...